Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi 'feki' mpita maduka ya 'spea' anaswa na kishoka wake

Polisi Feki Spare (600 X 238) Polisi 'feki' mpita maduka ya 'spea' anaswa na kishoka wake

Fri, 17 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam linamshikilia Frank Patrick Barnabas ambaye amekuwa akijifanya Askari Polisi huku akifanya uhalifu wa kutapeli Watu na kupita kwa Watu mbalimbali madukani kuwa anatafuta spea za pikipiki na magari ya Polisi akishirikiana na John Joseph Shija anayejifanya fundi wa magari ya Jeshi la Polisi.

“"Wamekua wakifika kwenye baadhi ya maduka Jijini Dar es salaam wakiomba Wamiliki wa maduka hayo washiriki katika kutoa misaada ya kutoa spea za magari na pikipiki za Polisi, taratibu za kisheria zinakamilishwa ili wafikishwe Mahakamani”

“Jeshi la Polisi linaendelea kuwashukuru Wananchi wanaoshiriki moja kwa moja katika ulinzi shirikishi, kutoa taarifa za Wahalifu na uhalifu na kuiishi falfasa ya Polisi jamii” amesema Kamanda Muliro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live