Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi bado wanamhoji Lema

97804 Lema+pic Polisi bado wanamhoji Lema

Wed, 4 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Singida. Mbunge wa Arusha Mjini nchini Tanzania  (Chadema), Godbless Lema anaendelea kuhojiwa na polisi mkoani Singida huku Chadema wakisema kuwa kada wao anatuhumiwa kwa kosa la kimtandao. Kauli hiyo inakuja ikiwa ni saa chache baada ya Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Sweetbert Njewike kusema kuwa mbunge huyo anahojiwa kwa tuhuma ya upotoshaji wenye lengo la kulichonganisha jeshi hilo na wananchi. Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Machi 3, 2020, Ofisa Uhamasishaji wa Chadema Mkoa wa Singida, Swaibu Mohamed amesema Lema anatuhumiwa kwa kosa la mtandao. “Lema bado anaendelea kuhojiwa na polisi mbele ya mawakili wake (Amani Mwiru na Hemed Nkulungu),”amesema Mohammed.

Chanzo: mwananchi.co.tz