Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi auawa kwa kuchomwa kisu alipokwenda kukamata wapika pombe za kienyeji

Hj6623569710 Polisi auawa kwa kuchomwa kisu alipokwenda kukamata wapika pombe za kienyeji

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Rumuruti nchini Kenya, ameuawa na wagemaji wa pombe za kienyeji maarufu kama chang'aa baada ya kumdunga kisu alipofika katika eneo wanalopikia pombe hizo.

Afisa huyo alidungwa kisu jana Alhamisi, Februari 16 alipofika katika eneo hilo akiwa kwenye bodaboda bila kujihami na silaha yoyote na kuanza kukabiliana na wagemaji hao.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Laikipia John Nyoike alisema kisa hicho kilitokea majira ya saa 2 usiku katika eneo la Maundu ni Meri.

"Imeripotiwa kuwa afisa huyo alipata taarifa kwamba kuna mitungi ya pombe iliyokuwa imeletwa eneo hilo, ndipo aliamua kuvamia eneo hilo," mkuu huyo wa polisi alisema.

"Mwendesha bodaboda ndiye alifika kuripoti kuwa mteja aliyepeleka eneo hilo alidungwa kisu baada ya ugomvi mkubwa kuibuka baina yake na mgemaji mmoja," ripoti hiyo iliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live