Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania yatoa sababu za kumshikilia mwandishi wa habari Bollen Ngeti

70723 NGETI+PIC

Sat, 10 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Polisi mkoa wa Ilala nchini Tanzania limetoa sababu za kumshikilia mwandishi wa habari za uchunguzi, Bollen Ngeti kuwa anatuhumiwa kumtukana mke wake na kumkashifu kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Agosti 9,2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Zuberi Chembera amesema mwandishi huyo anashikiliwa katika kituo cha polisi Buguruni, Dar es Salaam tangu jana Alhamisi walipomkamata.

Kamanda huyo amesema Ngeti alikamatwa baada ya mkewe kufungua kesi katika kituo cha polisi Buguruni akidai kutukanwa na kukashifiwa na mwandishi huyo.

Amesema kwa sasa kinachosubiriwa ni wadhamini wa mwandishi huyo kujitokeza na kukamilisha taratibu za dhamana kisha utaratibu mwingine wa kisheria utafuata.

Chanzo: mwananchi.co.tz