Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania yatoa sababu za kumkamata mwandishi wa habari

68923 Pic+kabendera

Tue, 30 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania imesema inamshikilia mwandishi wa habari za uchunguzi nchini humo, Erick Kabendera kwa mahojiano kuhusu uraia wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Julai 30, 2019, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema walimkamata Kabendera jana Jumatatu baada ya kupelekewa wito wa kufika polisi lakini akakaidi.

“Mwandishi huyo aliandikiwa barua ya wito kwa ajili ya mahojiano lakini alikaidi kutii wito huo. Kila mmoja anapaswa kutii wito bila sheria na kila mmoja anapaswa kutii ili kuondoa msuguano usiokuwa na lazima. Polisi tunapomwita kwa hiari akakaidi tunatumia mamlaka tuliyopewa kisheria,” amesema Mambosasa

“Baada ya kukamatwa, tumesikia taarifa mbalimbali na wengine waandishi wa habati wakisema ametekwa, niseme kuwa mwandishi huyo hakutekwa, aliitwa lakini kwa ujeuri akawa amekaidi wito huo,” amesema

Mambosasas amesema, “tunaendelea kuwasiliana na maofisa uhamiaji ili lile alilotuhumiwa nalo linawekwa mezani kwa yeye kuhakikishia hao wanaohoji Utanzania wake na ni lahisi kuthibitisha hilo.”

“Lakini kwa kuwa yeye mwenyewe ana mashaka, akakataa kutii sasa tunaye na taratibu zingine zinafuata,” huku akisema Kabendera anashikiliwa kituo Kikuu cha Polisi

Habari zinazohusiana na hii

Chanzo: mwananchi.co.tz