Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania yasema kigogo wa wizara ya fedha alijinyonga

69133 Pic+mambo+sasa

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Wakati Familia ya aliyekuwa ofisa mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe ikisema kifo cha ndugu yao hakikuwa cha kawaida, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kujinyonga kwa mtumishi huyo kupitia viashiria kadhaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Julai 31, 2019 kamanda wa polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema mazingira ya kujinyonga yanachaguzwa na kitendo cha kuacha wosia katika meza ofisini, akiwa ameeleza mgawanyo wa mali kwa watoto na ndugu zake.

Katika wosia huo, Mambosasa amesema uliagiza baadhi ya ng'ombe zake 25 alizokuwa anafuga, zitumike kitoweo katika msiba wake.

Lwajabe aliyekuwa mkurugenzi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini (EU) kupitia wizara hiyo, mwili wake ulikutwa wilayani Mkuranga mkoani Pwani Julai 26, 2019 ukining’inia juu ya mti wa mwembe kwa mujibu wa familia yake.

Kiashiria kingine alichokitaja Kamanda Mambosasa ni pamoja na mwili wake kutokuwa na majeraha yoyote huku akiwa amejisaidia haja kubwa. 

"Mtu yeyote akijinyonga lazima atatoa haja kubwa pamoja na mkojo, vyote hivyo vimekutwa eneo la tukio, tena akiwa hana jeraha lolote mwilini kwake, "amesema Mambosasa.

Habari zinazohusiana na hii

Baada ya mwili wa Lwajabe kukaguliwa eneo la tukio, alikutwa na Sh90,000 mfuko wa kushoto na Sh98,000 mfuko wa kulia na katika mfuko wa nyuma alikuwa na pochi yenye dola 10.

Chanzo: mwananchi.co.tz