Morogoro. Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro limekamata shehena ya vipodozi vyenye viambata vya sumu zilivyokuwa vikisafirishwa kutoka Zambia kuelekea Dar es Salaam.
Akizungumza leo Ijumaa Agosti 2, 2019 kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema maboksi 230 ya vipodozi hivyo yamekamatwa leo eneo la Chamwino barabara ya Morogoro- Iringa.
Amesema taarifa za kusafirishwa kwa vipodozi hivyo imetolewa na raia wema waliowapa habari polisi waliokuwa doria katika barabara hiyo, kuliwekea gari hilo kizuizi ambalo pia lilikuwa limepakia mchanga wa shaba.
Kamanda Mutafungwa amemtaja dereva wa gari hilo kuwa ni Sudi Mnukwa na msindikizaji wa vipodozi hivyo Samson Emanuel wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
Amebainisha kuwa baada ya kuhojiwa walieleza kuwa vipodozi hivyo walivipakia Tunduma ambako ni mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Amesema kuwa pamoja na kuwashikilia watuhumiwa hao, gari lililobeba vipodozi hivyo limezuiwa.
Pia Soma
- Mwanaharakati jela Uganda miezi 18 kwa kumtusi Museveni
- Katy Perry kulipa fidia ya Sh6 bilioni kwa kunakili wimbo
- Waziri azungumzia awamu ya tatu Tasaf, asema kaya zote masikini kumulikwa
- Waziri Ummy azindua huduma ya dharura kwa wagonjwa mahututi