Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania, Interpol wamkata aliyewatapeli watalii

Pingu?fit=800%2C445 Polisi Tanzania, Interpol wamkata aliyewatapeli watalii

Sun, 28 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi limesema limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyewatapeli watalii waliokuja nchini kwa ajili ya kupanda Mlima Kilimanjaro, huku likibainisha kuwa Tanzania ni nchi salama kwa wageni wa ndani na nje ya Tanzania.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Maigwa,  katika lango la Mweka, ambalo hutumika kushuka kutoka katika Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu barani Afrika.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa aliyekamatwa jina jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiupelezi, huku akibanisha kuwa mtuhumiwa  anatoka nje ya Tanzania, huku akiwaomba watalii hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania.

Kwa upande wake Bw. Chris Lomas ambae ni Mkurungenzi wa  kampuni ya hope for love, ameishukuru serikali na Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo wamelifuatilia swala hilo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliye watapeli.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live