Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tabora yawasaka watuhumiwa wa ubakaji

Wed, 10 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Watu wawili wamebakwa katika matukio mawili tofauti, akiwemo mtoto mwanafunzi mwenye umri wa miaka minane.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema leo Jumanne Aprili 9, 2019 kuwa matukio hayo yametokea katika Manispaa ya Tabora.

Amesema katika tukio la kwanza mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mabatini (jina linahifadhiwa),amebakwa na kulawitiwa na mtu ambaye kwa sasa jina lake Polisi wanalihifadhi ili kutoharibu ushahidi.

Amesema mtu huyo akitajwa anaweza kukimbia kwani anatafutwa kujibu tuhuma zinazomkabili.

Amesema jana saa saba mchana walipata taarifa kuwa katika eneo la Hospitali ya Mtakatifu Phillipo kuwa kuna mtu amemfanyia vitendo viovu mwanafunzi mwenye umri wa miaka minane.

Ameeleza mtu huyo bado hajapatikana na polisi inamtafuta ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

Katika tukio la pili mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina moja la Anthony anadaiwa kumbaka mtu ambaye anahifadhiwa jina lake na kukimbia.

Kamanda Nley, amesema mtuhumiwa baada ya kubaka, alikimbia na Jeshi la Polisi linamtafuta.



Chanzo: mwananchi.co.tz