Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Mwanza wakamata watuhumiwa 264

Mbaroni?fit=1000%2C563&ssl=1 Polisi Mwanza wakamata watuhumiwa 264

Sun, 16 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kukamata watuhumiwa 264 wa makosa mbalimbali ya uhalifu katika kipindi cha siku 13 na wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu makosa yanayowakabili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mtafungwa alisema hayo jana jijini Mwanza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika misako ya kuanzia Machi 31 hadi Aprili 14, mwaka huu katika maeneo tofauti mkoani humo.

Aliyataja makosa hayo kuwa ni kukutwa na mirungi, wizi wa mtoto, wizi wa mafuta ya dizeli, simu mbalimbali na mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na kuendesha vyombo vya moto bila kufuata sheria.

Alisema Aprili 14, mwaka huu maeneo ya Kitongoji cha Nyankololo, Kijiji cha Nyamtelela, Wilaya ya Sengerema kuliripotiwa taarifa ya kuibiwa mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi mitatu na watu wasiojulikana.

Baada ya taarifa hizo kuripotiwa kituo cha polisi, askari walianza ufuatiliaji na ilipofika Aprili 8, mwaka huu walifanikiwa kumkamata Sara Robert (33) mkulima, mkazi wa Nyashitale akiwa na mtoto huyo na mama mzazi wa mtoto huyo aliweza kumtambua kuwa ndiye aliyekuwa ameibwa.

Alisema baada ya mahojiano ya kina, Sara alikiri kuhusika na wizi wa mtoto huyo na kudai kuwa alitaka kwenda kumridhisha mume wake kwa kumhadaa kuwa amepata mtoto wa kiume kwani watoto aliobahatika kuwa nao wote ni wa kike.

Kamanda Mtafungwa alisema afya ya mtoto inaendelea vizuri pamoja na uchunguzi mwingine umefanyika na amekabidhiwa kwa wazazi wake kwa malezi.

Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo mara baada ya kukamilishwa kwa upelelezi.

Kamanda Mtafungwa aliwataka wananchi wote kufuata sheria za nchi ili kuepukana na makosa ambayo yanawapelekea kukumbana na mkono wa dola.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live