Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Moro waanza uchunguzi kifo cha mfugaji wa kimasai

49380 POLIS+PIC

Fri, 29 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema tayari wamefungua jalada la uchunguzi kufuatia tukio la mauaji ya mfugaji wa jamii ya kimasai Lepeti Mandero (20) mkazi wa kijiji cha Mtakuja Mvomero aliyeuawa na askari wa Jeshi la Magereza Mbugiri baada ya kuingiza mifugo ndani ya shamba la gereza.

Kamanda Mutafungwa ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa Machi 29, 2019 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo pia amesema askari wanne wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi huku akiwataka wazazi na wananchi kuwa wavumilivu na kulichia jeshi la polisi kufanya uchunguzi.

Amewataja askari hao kuwa ni mwenye namba A6106 SGT Roma, B6064 Coplo Barnabas, B6942 Wada Albart na B8796 Wada Tatius ambao wote ni askari wa Gereza la Mbigiri lililopo wilaya ya Kilosa.

Akizungumzia tukio lilivyotokea Kamanda Mutafungwa amesema Machi 27, 2019 askari hao wanne wakiwa kwenye operesheni ya kuondoa mifugo ndani ya shamba la miwa la Magereza ghafla walimuona marehemu akiwa na makundi mawili ya ng’ombe na walipojaribu kuzuia ng’ombe ndipo marehemu na wenzake walipoanza kuwashambulia askari hao kwa sime, rungu na fimbo.

Amesema katika mapambano hayo askari magereza walianza kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya lakini marehemu na wenzake waliendelea kuwashambulia na ndipo askari mmoja alipofyatua risasi na kumjeruhi kiunoni karibu na tumbo na kusababisha kifo cha mfugaji huyo.

Kamanda Mutafungwa amesema tayari mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi wa kidaktari na ndugu wameshauchukua na tayari umezikwa.

Ametoa wito kwa wananchi kutoingia na kufanya shughuli za kilimo, ufugaji na nyingine za kibinadamu kwenye maeneo ya Serikali, majeshi na kwenye maeneo ya hifadhi.

 Soma zaidi>> Askari Magereza adaiwa kumuua mfugaji kwa kumpiga risasi, baba agoma kuzika mwanae



Chanzo: mwananchi.co.tz