Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi: Mlioibiwa Simu, TV fikeni 'Sentro' kutambua mali zenu

Simu Za Wiziiii Polisi: Mlioibiwa Simu, TV fikeni 'Sentro' kutambua mali zenu

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amewataka wananchi walioibiwa simu na vifaa vingine vya kielektroniki kama vile runinga, kompyuta na redio kufika katika kituo cha polisi cha Sentro kwa ajili ya kuzitambua mali zao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba 19, 2023 kituoni hapo, Muliro amesema mali hizo zimekamatwa katika oparesheni maalum iliyoanza Septemba ambapo wamefanikiwa kuwakamata wahalifu 27.

"Watu waje kuzitambua mali zao. Tumekamata kompyuta mpakato 10, Simu za mkononi 305, runinga 36, makava ya simu 160, kamera 4 na redio (subwoofer) 3, amesema Muliro.

Amesema tayari baadhi ya mali hizo zimeshatambuliwa na hatua za kuwashughulikia wahalifu kwa mujibu wa sheria zinaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live