Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Polisi Mlandizi wanadaiwa kuhujumu mradi SGR'

3dc64a99a1bb8865ff6c537ba8953cce.jpeg 'Polisi Mlandizi wanadaiwa kuhujumu mradi SGR'

Thu, 10 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS John Pombe Magufuli amesema amesikitishwa na Polisi wasio waaminifu kuhujumu miundombinu ya reli ya kisasa 'SGR'.

Rais Magufuli ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa uapisho wa Mawaziri na Naibu Mawaziri ambapo amesema juzi walikamata magari nane yaliyokuwa yakisomba vyuma vya reli.

"Tumekamata magari nane yanayosomba vyuma, wanaita chakavu wakati ni vyuma vya SGR, na baadhi ya washiriki ni Mkuu wa Polisi Mlandizi(Mkoa wa Pwani), OCD na wasaidizi wake.

"Fikiria vyuma vya shilingi trilioni saba na pointi vya kujenga reli alafu watanzania wachache wanaiba wanaenda kuuza kwa bei ndogo kwenye viwanda vya Nondo.

"Kituo cha Polisi Mlandizi OCD na watendaji wake nimeagiza waondolewe, IGP natumahi umeshaondoa,” alisema Rais Magufuli.

Chanzo: habarileo.co.tz