Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limepiga marufuku maandamano yanayoashiria uvunjifu wa amani na kuwataka wananchi kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kuepuka kuvunja sheria.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi ametoa agizo hilo leo mara baada ya kumaliza mazoezi ya utayari kwa Jeshi la polisi ikiwa ni kuelekea mwisho wa mwaka huku akitoa salama kwa watu wanaojihusisha na uhalifu kuacha mara moja.
Katika hatua nyingine kamanda Magomi amewataka watumiaji wa vyomba vya usafiri ikiwemo vyombo binafsi, umma na serkali kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani ili kuzuia ajali za barabarani ambazo hukithiri katika kipindi cha mwisho wa mwaka.
Kamanda Magomi amesema jeshi hilo limeendelea kujipanga kuhakikisha usalama wa raia na mali zao na kupiga marufuku maandamano na mikusanyiko inayoashiria vurugu mkoani humo.