Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Kilimanjaro yanasa gari linalodaiwa kuibwa Dar

DA452542 7DEE 4F43 BDED 7950DD2EB3D6.jpeg Polisi Kilimanjaro yanasa gari linalodaiwa kuibwa Dar

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja ambaye ni mkazi wa Moroco, jijini Dar es Salaam kwa kukutwa na gari ya wizi aina ya Toyota RAV4 aliyokuwa akiiendesha kwenda nayo jijini Arusha.

Mtu huyo ambaye jina lake limehifadhiwa na polisi kwa sababu za kiuchunguzi, alikamatwa usiku wa kuamkia Desemba 26, 2022 katika doria iliyokuwa ikifanywa na jeshi hilo katika Wilaya ya Mwanga, mkoani humo. Akizungumza jana Jumatano, Desemba 28, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Simon Maigwa amesema zipo operesheni ambazo zinafanyika maeneo mbalimbali ya mkoa huo na kwamba Desemba 26 askari wakiwa doria Wilaya ya Mwanga walifanikiwa kulikamata gari hilo.

Maigwa amesema baada ya kulikamata gari hilo, walilifanyia ukaguzi na kubaini kuwa na injini namba SAZ0011413 na chassis namba ACA315005590 kisha walimkamata mtuhumiwa huyo na kumfikisha katika Kituo cha Polisi Mwanga.

"Desemba 26 mwaka huu majira ya usiku askari wa Wilaya ya Mwanga wakiwa doria walifanikiwa kuikamata gari iliyokuwa imeibwa kutoka Jijini Dar es Salaam kupelekwa Arusha na bahati tulimkamata mtuhumiwa na tunaye," amesema RPC Maigwa.

Kamanda Maigwa amesema taratibu za kumrudisha mtuhumiwa huyo na kielelezo hicho (gari) kuelekea jijini Dar es Salaam zinafanyika ili taratibu nyingine za kisheria ziendelee.

Chanzo: Mwananchi