Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Kigoma yawataka waliopiga kura kurejea majumbani

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kakonko. Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno, amesema zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa ubunge jimbo la Buyungu mkoani hapa linaendelea vizuri na kuwataka wananchi kurejea majumbani mara baada ya kupiga kura.

Kamanda Ottieno ametoa kauli hiyo leo Jumapili Agosti 12, 2018 na kubainisha kuwa ulinzi umeimarishwa vizuri katika vituo vyote vya kupigia kura katika jimbo hilo.

Amesema mpaka sasa hakuna taarifa walizopata za kutishia usalama wa uvunjifu wa amani na hali ipo shwari.

Amesema ni vyema wananchi watakapomaliza zoezi la kupiga kura wakarudi nyumbani ili kuepusha msongamano katika vituo usio na sababu.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz