Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Kigoma waua washukiwa 12 wa ujambazi

75694 Mauaji+pic

Mon, 16 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibondo. Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limewaua washukiwa 12 wa ujambazi waliodaiwa kuwa katika mpango wa kuteka magari katika kijiji cha Kilemba wilayani Kibondo.

Akizungumzia kijijini hapo jana Ijumaa Septemba 13, 2019 Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Otieno amesema siku za hivi karibuni kumeibuka matukio ya utekaji magari, baadhi ya waliokamatwa walieleza matukio hayo.

Amesema polisi walifika eneo hilo na kuanza kurushiana risasi na watu hao na kuwaua 12 waliokutwa na bunduki tatu aina ya AK 47, risasi 107, mapanga, visu na mabomu matatu ya kurusha kwa mkono.

‘’Licha ya kuwa wananchi wa Burundi wanajihusisha na ujambazi, hapa nchini natoa onyo kwa Watanzania wanaowakaribisha watu hawa ukibainika utachukuliwa hatua.”

“Wengi wamegeuza mkoa wa Kigoma kuwa sehemu salama kwao kwa kufanya mambo yao yasiyofaa sasa tutamshughulikia kila mtu ambaye hataki kufuata sheria za nchi yetu awe mgeni au mwenyeji,” amesema Otieno.

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz