Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, ametoa onyo kali kwa wanaojihusisha na uhalifu katika kata ya Pamba wilaya ya Nyamagana, akiwataka kuacha mara moja na kujisalimisha kwa sababu oparesheni kali inaanza katika mtaa huo huku akisisitiza kuwa hawatanii wala hana utani na wahalifu.
Kamanda Mutafungwa amesema hayo baada ya malalamiko ya wananchi wa kata hiyo juu ya watu wanaojihusisha na vitendo vya uporaji, ubakaji, matumizi ya madawa ya kulevya na wanaovunja nyumba zao.
"Narudia kusema ole wenu, na mimi nina bahati mbaya huwa sitanii, nimeelimisha nimemaliza hii kauli yangu ya mwisho niliyoitoa kuhusu wahalifu wala sitanii, kwa sababu sijaja hapa kuwatania, mimi siyo mtani wenu na sijawahi kuwatania" amesema Kamanda Mutafungwa.