Tue, 18 Jun 2019
Chanzo: mwananchi.co.tz
Geita. Polisi mkoani Geita linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kujifanya ni maofisa usalama wa Taifa kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Watu hao ambao ni wakazi wa jijini Dar es Salaam walikamatwa Juni 11,2019 baada ya kuingia soko la dhahabu lililopo mjini Geita na kujitambulisha ni kutoka usalama wa Taifa wanaofuatilia masuala ya kodi
Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Juni 18, 2019 Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amewataja watuhumiwa hao ni Alfred Disapeter (33) Steven Katunzi (36) na Ester Mwakilasa(32) wote wa jijini Dar es salam
Chanzo: mwananchi.co.tz