Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi: Diwani aliyepotea tangu Feb, 2022 apatikana kwa Mwanamke Tabata

MULIROro Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi DSM

Tue, 24 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusu Diwani wa Kata ya Kawe Mutta Rwakatare (43) Mkazi wa Mikocheni Kinondoni kutojulikana alipo tangu mwezi wa pili mwaka 2022, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Muliro Jumanne amesema Diwani huyo amepatikana akiwa kwa Mwanamke aitwae Ashura ambaye amedai kuwa ni Rafiki yake.

"Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam lilifanya ufuatiliaji wa taarifa hizo na kufanikiwa kumpata Diwani huyo tarehe 23/05/2022 akiwa kwenye nyumba ya Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Ashura Ally Matitu, miaka 43, Mzaramo mkazi wa Tabata darajani ambaye alidai kuwa Diwani huyo ni rafiki yake wa siku nyingi kwa zaidi ya miaka 10 na alifika nyumbani kwake tarehe 19/05/2022 huku akiwa katika hali ya ulevi uliopindukia"

"Kutokana na mazingira ya ulevi ambayo Diwani huyo amekutwa nayo na maombi yaliyotolewa na ndugu zake kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya matibabu, ndugu pia walitoa kumbu kumbu za nyuma, mwenendo na tabia za Diwani huyo hivyo Jeshi la Polisi limemkabidhi diwani huyo kwa ndugu zake kwa matibabu na tiba zaidi za kisaikolojia" ——— Jumanne Muliro Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM

Chanzo: www.tanzaniaweb.live