Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Dar wakamata watatu na meno ya tembo

Meno Ya Tembo Polisi Dar wakamata watatu na meno ya tembo

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa watatu kwa kuwakuta na vipande 25 vya meno ya tembo.

Pia, Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 29 kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Machi 9, 2022, Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema tangu Februari 25 hadi Machi 9, wamekuwa wakisimamia operesheni maalum ya kuzuia uhalifu.

Amesema polisi ikishirikisha Kikosi Kazi cha Kuzuia na kupambana Ujangili katika eneo la Ubungo NHC walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watatu ambao ni Gabriel Mgana, mkazi wa Ubungo NHC 2, Haffarman Yona, mkazi wa Kinyerezi na Felician Cyril mkazi wa Kinyerezi.

Amesema watu hao walikamatwa wakiwa na vipande 25 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kg 20 sawa na Tembo 14 waliouawa.

Kamanda Muliro amebainisha kuwa vipande hivyo vilifichwa ndani ya nyumba ya mmoja wa watuhumiwa hao.

“Pia Gari aiana ya Toyota Wiills inayodaiwa kutumika kusafirisha meno hayo hapa Dar es salaam imekamatwa. Uchunguzi wa kina unafanywa kujua Tembo waliouawa ni wa eneo lipi na thamani ya meno hayo ni kiasi gani na yalikuwa yanatarajiwa kupelekwa au kuuzwa wapi,” amesema.

Vilevile amesema operesheni hiyo pia imewanasa Khatib Abdala (33) mkazi wa Banana Kitunda, na wenzake watatu kwa tuhuma za wizi kwa njia ya mtandao katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam.

“Upekuzi wa kina ulifanyika katika nyumba za watuhumiwa hao na walikutwa na jumla ya kadi (line) za simu 46 za kampuni tofauti tofauti, Vizibao 4 vya uwakala wa kusajilia line (freelancer) Simu za mkononi 14 na Vitambulisho vitatu vyenye majina yasiyo yao wanavyotumia katika kazi zao za kusajili line na hatimaye kuwaibia wateja.

“Pia Askari Polisi walimefanikiwa kuyapata Magari matatu ambayo ni aina ya Nisan Extray, Passo na Toyota Prado ambayo yaliibwa jijini kwa nyakati tofauti. Upelelezi wa kina kuwapata watu wote wanaojihusisha na wizi wa Magari unaendelea,” amesema.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za wizi wa vitu vya kielektoniki zikiwemo Luninga bapa (TV flat screen) nne zenye ukubwa wa nchi 35, 65, 75 na 85, Generator kubwa 1, Mitungi ya gesi 3, feni 2,

Lap top HP 2 Samsang 1 na piki piki moja aina ya TVS yenye namba za usajili MC 338 DAH.

“Watuhumiwa wengine 17 walikamatwa pia kwa makosa ya kupatikana na Bhangi kiasi cha Masanduku ya chuma 2 (tranker 2), Nusu gunia, Puli 810, Kete 1305 na Misokoto 670. Aidha watuhumiwa wawili walikamatwa kwa kosa la kupatikana na mitambo minne ya kutengezea pombe ya moshi, lita 780 ya pombe hiyo.

“Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa na linaahidi kuzitunza na kuzifanyia kazi kwa siri,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live