Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi, DPP watupiana lawama kesi kuchelewa mahakamani

Polisi, DPP Watupiana Lawama Kesi Kuchelewa Mahakamani Polisi, DPP watupiana lawama kesi kuchelewa mahakamani

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wakati kukiwa na malalamiko ya ucheleweshaji wa kesi za udhalilishaji mahakamani, Kamishana wa polisi Zanzibar, Hamad Khamis Hamad amesema Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mkurugezi wa Mashtaka (DPP) wameanza kunyosheana vidole ucheleweshaji wa kesi hizo.

Ametoa kauli hiyo jana Jumatano Agosti 24, 2022 wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Mtandao wa Utetezi Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kwa jeshi la polisi na ofisi ya DPP Zanzibar kuhusu utii wa sheria.

“Baada ya mafunzo haya twende tuboreshe upungufu uliopo katika kuchelewesha upelelezi na uendeshaji wa kesi mahakamani, lazima niwe wazi tumeanza kutupiana mpira katika kesi za udhalilishaji,” amesema Kamishan Hamad.

Hata hivyo, amesema ipo haja ya wadau wa haki jinai kukaa pamoja na kutoa elimu zaidi kuhusu suala hilo na kila mmoja kutambua mipaka yake ya kazi kuanzia kwenye ukamataji, kupeleleza na kuendesha kesi mahakamani.

Amesema yapo malalamiko ambayo siyo rasmi kuwa upande wa polisi wakipeleka jalada hilo kwa DPP kwa ajili ya kuendelea na kesi lakini mtuhumiwa anaitwa mara nyingine kuanza kuhojiwa kitendo ambacho kinaweza kuibua hisia za kutaka kupoteza ushahidi.

Naye Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema polisi wanawajibika moja kwa moja kulinda na kutetea haki za binadamu tangu wanapokamata na kupeleleza

Alisema hata mwananchi anapopata tatizo sehemu ya kwanza hukimbilia polisi lakini wakati mwingine hujikuta wakiptia wakati mgumu 

Rashida Ahmed Suleiman kutoka ofisi ya DPP Zanzibar amesema  dhana ya haki zabinadamu ni pana hivyo hakuna namna wanaweza kuikwepa kwasababu kila siku wanashughulika na masuala yanayohusu haki hizo.

“Tunapaswa kuzingatia haki za binadamu, wakati wa kuendesha kesi lazima tuzingatie misingi na haki hizo,” amesema

Kutokaana na uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na kulalamikiwa na vyombo vya dola, THRDC imetoa mafunzo ya siku mbili kuhusu utawala wa sheria.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz