Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Arusha wanasa watuhumiwa wa utengenezaji fedha bandia

37374 Pic+fedha Polisi Arusha wanasa watuhumiwa wa utengenezaji fedha bandia

Sun, 20 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha . Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewakamata watuhumiwa sita kwa makosa mbalimbali.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Ng'anzi amesema leo Ijumaa Januari 18, 2019 kuwa watuhumiwa wanne ambao hakuwataja majina yao kwa sababu za kipelelezi wanajihusisha na utengenezaji wa fedha bandia.

Amesema mtuhumiwa wa kwanza alikutwa na noti bandia za dola 50 za Marekani (Sh112,500) zenye thamani ya dola 500 (zaidi ya Sh 1.1 milioni).

"Huyu mtuhumiwa wa kwanza aliwapeleka askari wetu nyumbani kwake eneo la Daraja Mbili ambako zilikutwa fedha bandia za mataifa mbalimbali," amesema Ng'anzi

Fedha hizo ni dola za Marekani, fedha za Umoja wa Ulaya (Euro), Kenya, Malawi, Zambia, Rwanda na Sudan.

Amesema watuhumiwa wanashikiliwa kwa ajili ya mahojiano na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, Ng'anzi amesema kuwa watuhumiwa wengine wawili ambao ni Kennedy Mbilinyi na Richard Loishiye wamekamatwa kwa kuiba gari aina Harrier lenye namba za usaili T 241 DKC na kujaribu kulivusha mpaka wa Namanga kuelekea nchi jirani ya Kenya.



Chanzo: mwananchi.co.tz