Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Arusha bado wamshikilia hakimu anayedaiwa kumlawiti bodaboda

Hukumu Pc Data Polisi Arusha bado wamshikilia hakimu anayedaiwa kumlawiti bodaboda

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Mkoa wa Arusha inaendelea na uchunguzi wa tukio la Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Loliondo wilayani Ngorongoro, anayedaiwa kumlawiti kijana baada ya kumlewesha.

Kwa mujibu wa Polisi, hakimu huyo anaendelea kushikiliwa, huku kijana huyo (29) ambaye ni mwathirika wa tukio hilo akiachiwa.

Akizungumza leo Jumatano Februari 7, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema: “Kwa sasa kinachoendelea ni uchunguzi wa tukio hilo na mtuhumiwa ndiye tunaendelea kumshikilia hadi sasa.”

Hadi juzi, Februari 3,2024 mbali na hakimu huyo, polisi pia ilikuwa inamshikilia mwathirika wa tukio hilo kutokana na msimamo wa sheria unaotaka mwanamume anayemruhusu mwanamume mwenzake kumwingilia (unnatural), ametenda kosa la jinai.

Inadaiwa tukio hilo limetokea Februari 2, 2024 kati ya saa tatu na saa nne usiku nyumbani kwa kijana huyo ambaye hufanya kazi ya kuendesha pikipiki maarufu bodaboda katika eneo la Wasso wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

Inadaiwa hakimu huyo ambaye hivi karibuni alihamia kikazi, alionekana mchana akiwa na kijana huyo na baadaye jioni walienda kunywa pombe nyumbani kwa kijana huyo.

“Ilipofika usiku kaka yake na kijana aliyelawitiwa (jina linahifadhiwa) alifika nyumbani kwa mdogo wake na kuwakuta wakiwa uchi, ndipo alipompigia simu hakimu mwenzake na mtuhumiwa," kimedai chanzo cha taarifa na kuongeza:

"Alipokuja huyo hakimu mwenzake, walipiga simu polisi ambao walikuja kuwachukua wote wawili na hadi sasa wanashikiliwa kituoni."

Chanzo hicho cha taarifa kimesema kijana huyo katika mahojiano ameeleza ni mara ya tatu hakimu huyo kumfanyia kitendo hicho na kuwa aliamua kunyamaza kwa madai aliona kutoa taarifa ingemdhalilisha.

Alipelekwa hospitali ya Wasso kwa matibabu na daktari kuthibitisha ameingiliwa.

Taarifa zinadai hakimu huyo alikuwa na mazoea na kijana huyo kutokana na kumtuma mara kwa mara, ikiwamo kumsafirisha kutoka eneo moja kwenda lingine kwa kutumia pikipiki yake.

Imeelezwa kijana huyo aliachiwa na polisi Februari 4, 2024 na anaendelea na shughuli zake za bodaboda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live