Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pingamizi la Jamhuri kesi ya Sabaya latupwa

Sabaya 2 Pingamizi la Jamhuri kesi ya Sabaya latupwa

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imetupilia mbali pingamizi la Mawakili wa Jamuhuri kupinga kupokelewa kwa kielelezo cha shahidi wa 10.

Maamuzi hayo adogo yametolewa leo Jumanne Desemba Mosi, 2021 wakati wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Lengai Ole Sabaya na wenzake sita ikiendelea.

Maelezo ya shahidi wa Jamhuri, Francis Mrosso yalidaiwa kutofautiana na maelezo aliyoyatoa polisi na mahakamani.

Katika kielelezo hicho cha maelezo yaliyotofautiana ni idadi ya vijana waliokuwa na Mrosso alipokwenda kutoa fedha benki ya CRDB tawi la Kwa Mrombo jijini Arusha, umri wa shahidi huyo na namba ya mlipakodi (TIN number).

Katika maelezo hayo, inaonyesha kuwa akiwa kituo cha polisi shahidi, alisema ana miaka 47 na jana mahakamani alisema ana miaka 44, pia tofauti nyingine ni namba ya mlipakodi katika kielelezo cha polisi imepungua namba Moja.

Hata hivyo hoja hiyo ya kupokelewa kielelezo hicho chenye mapungufu imepingwa vikali na Mawakili wa Jamhuri wakiongozwa na Wakili Mwandamizi Tarsila Gervas ambapo ameiomba mahakama kutopokea kielelezo hicho kwa kuwa kimekiuka matakwa ya uwasilishaji katika Sheria ya ushahidi.

Hata hivyo hoja hiyo ya kupokelewa kielelezo hicho chenye mapungufu imepingwa vikali na Mawakili wa Jamhuri wakiongozwa na Wakili Mwandamizi Tarsila Gervas ambapo ameiomba mahakama kutopokea kielelezo hicho kwa kuwa kimekiuka matakwa ya uwasilishaji katika Sheria ya ushahidi.

Wakili Tarsila alieleza mahakama kuwa kielelezo hicho kilipaswa kifuate utaratibu hata kama shahidi amekubali kitumike mahakamani hivyo hakiwezi kukiuka Sheria na kupokea kielelezo chenye makosa.

Hakimu Kisinda amesema mahakama imetupilia mbali pingamizi hilo la mashtaka kwa kuwa haliendani na matakwa ya Sheria ya ushahidi.

Katika kesi hiyo, watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Chanzo: mwananchidigital