Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pikipiki yawafikisha kortini watu wanne

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Dar  es Salaam nchini Tanzania wakikabiliwa na shtaka moja la wizi wa pikipiki

Washitakiwa hao ni Juma Saidi (35), Abdallah Alifani (39), Ramadhani Selemani (39) na Rehema Abdalah (22).

Wakili wa Serikali Veronika Mtafya amedai jana Jumanne Julai 30, 2019 mbele ya Hakimu Lihamwike  Boniphace kuwa Julai 8,2019  maeneo ya mikocheni Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam washtakiwa hao waliiba pikipiki namba MC 237 yenye thamani ya Sh2,250,000 mali ya Elisha Bagarama.

Wakili Mtafya alidai washtakiwa hao kabla na baada ya kuiba walimtishia Ibrahimu Abdul, kwa kutumia bastola huku akisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwaajili ya kutajwa.

Naye wakili wa utetezi, Samweli Ntabalia aliomba upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi mapema.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Lihamwike aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 13,2019 na washtakiwa wamepelekwa rumande kwa kuwa shitaka linalowakabili  halina dhamana.

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz