Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pikipiki ilivyosababisha wafanyabiashara watatu kuuawa

Kifo Kifo Mauiaji.png Pikipiki ilivyosababisha wafanyabiashara watatu kuuawa

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara watatu katika machinjio ya Mazizini yaliyopo Ukonga Mombasa, wameuawa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi wakiwatuhumu kupora pikipiki eneo la Pugu Kinyamwezi jijini Dar es Salaam.

Mauaji hayo yametokea leo Februari 7, 2024 saa 10 alfajiri baada ya wafanyabiashara hao kukaswa wakitumia pikipiki hiyo inayodaiwa ya wizi.

Imedaiwa kuwa wafanyabiashara hao, akiwemo aliyetambuliwa kwa jina moja la Jeremia anayemiliki bucha eneo la Namanga, walipora pikipiki wiki iliyopita.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amezungumzia tukio hilo akisema mmoja wa wafanyabiashara hao ndiye aliyepora pikipiki hiyo eneo la Pugu Kinyamwezi.

Kamanda Murilo amesema wananchi wa eneo hilo walikuwa wanaifuatilia, ndipo walipofika eneo lenye mlima, jirani na Shule ya Sekondari Pugu, walipokuwa kwenye mteremko walitaka kuruka ili wakimbie, lakini walikamatwa na pikipiki hiyo.

“Katika harakati za wananchi kuwatandikatandika, inadaiwa wakati wanaelekea hospitali walifariki dunia lakini aliyekabwa yupo na pikipiki iliyoibwa, nayo imepatikana. Hizo ni taarifa za awali,” amesema.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Samwel Nasphory

amesema saa 10 alfajiri akiwa stendi eneo la Sekondari ya Pugu alisikia kelele zinazoita mwizi, mwizi kwenye mteremko wa mlima.

Amesema alishuhudia watu wakipigwa, huku wengine wakiwasha moto ili kuwachoma.

“Kati ya wafanyabiashara watatu mmoja alitambuliwa palepale wakimtaja kwa jina moja la Jeremia ambaye inadaiwa alinunua pikipiki ya wizi na ana bucha za nyama eneo la Namanga,” amesema.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Pugu Bombani, Amani Bungara amesema alipigiwa simu saa 11 alfajiri kwamba, kuna wafanyabiashara watatu wameunguzwa moto.

Amesema alipofika eneo la mlima wa sekondari ya Pugu alikuta watu hao wameuawa.

Bungara amesema mashuhuda aliowakuta eneo hilo walidai watu hao waliunguzwa moto saa 10 alfajiri wakiwa na pikipiki inayodaiwa ya wizi.

“Pikipiki hiyo ilinunuliwa na mmoja wao waliyemtaja Jeremia, na inadaiwa bodaboda walikuwa wanaifuatilia kila inapoenda,” amesema Bungara.

Amesema Polisi wafika eneo hilo na kuchukua maelezo, ikielezwa kuwa watu hao ni wafanyabiashara wa ng’ombe katika machinjio ya Mazizini Ukonga na wanaishi Majohe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live