Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Peter Kibatala awasili Mbeya kumtetea Sugu

2835 Kibatala 536x400

Fri, 9 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo February 8, 2018 Wakili maarufu nchini Peter Kibatala amewasili katika jiji la Mbeya ili kuwawakilisha Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Emmanuel Masonga

Sugu na Masonga wanakabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambayo wanadaiwa kuitoa December 30, 2017 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea leo kwa Sugu na Masonga kuanza kutoa utetezi wao chini ya wakili wao mpya Kibatala baada ya mawakili wao wa awali, Boniface Mwakubusi, Sabina Yongo na Hekima Mwasipu kujitoa katika kesi hiyo.

WEMA SEPETU ALIVYOFIKA MAHAKAMANI KISUTU NA WAKILI MSANDO

Chanzo: millardayo.com