Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Pepo’ afungwa maisha kwa kumlawiti mtoto

Hukumu Pc Data ‘Pepo’ afungwa maisha kwa kumlawiti mtoto

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limewafikisha mahakamani zaidi ya watuhumiwa 76 wakiwa na makosa mbalimbali ambapo baadhi ya kesi hizo zilishapatikana na hatia na watuhumiwa kufungwa akiwemo Justine Allex (21) almaarufu (pepo) mkazi wa Kijiji cha Njenga Wilayani Masasi aliyefungwa kifungo cha maisha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kaimu Kamada wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mtaki Kurwijila amesema kuwa mnamo Oktoba 11 mtuhumiwa Justine alifungwa kifungo cha maisha kwenda jela baada ya Mahakama ya Wilaya ya Masasi kumtia hatiani kwa kosa la kulawiti mtoto wa darasa la pili.

Anasema kuwa mnamo Julai 1 saa 9 alasiri katika Kijiji cha Njenga mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi baada ya kumlawiti mtoto wa kiume (8) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili baada ya kumpeleka porini kisha kumfunga kamba na kuanza kumlawiti.

Jeshi la Polisi ili kukomesha kabisa matukio ya kiharifu hususani unyanyasaji wa kinsia na watoto hatua kali kisheria zitaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa mkoa unaendelea kuwa shwari bila vitendo vya uharifu.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limekamata watu 27 kwa makosa mbalimbal ikiwemo kukutwa na bangi kilo 8 na gramu 183, na pombe ya moshi lita 619.5.

Aidha, jeshi hilo linatoa elimu ya kupambana na uharifu kwa wananchi na imeendelea kuleta mwitikio mkubwa kwa wananchi zikiwemo doria na misako iliyofanyika tangia Oktoba 1, 2023 hadi Oktoba 31, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live