Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Pemba wakati tunasambaza masanduku ya kupigia kura Polisi walirushiwa mawe"

Screenshot 2020 10 27 At 14.19.10 660x400.png "Pemba wakati tunasambaza masanduku ya kupigia kura Polisi walirushiwa mawe"

Tue, 27 Oct 2020 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Jeshi laPolisi nchini, IGP Simon Sirro ametoa wito kwa watanzania katika kipindi hiki chauchaguzi kujihadhari na mihemko isiyokuwa na tija inayoweza kuwaletea matatizo.

Akizungumza nawaandishi wa habari hii leo, Sirro amesema kila mtu anategemewa na familia yake, hivyo ni vyema kuepuka vurugu zinazoweka kuharibu amani iliyopo.

“Kama unajua hutopiga kura usiwe sehemu ya kuanzisha vurugu kwakuwa hapo jana usiku huko Pemba kipindi tunasambaza masanduku ya kupigia kura Polisi walirushiwa mawe hivyohatutarajii kujirudia” Sirro.

Amesema kunamaisha baada ya uchaguzi na kwamba ushindani wowote lazima mmoja ashindena hata kama aliyeshinda ni adui yako unatakiwa uvumilia.

KAMANDA MBEYA ATOA ONYO KUELEKEA UCHAGUZI

Chanzo: millardayo.com