Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paroko mbaroni akidaiwa kughushi, kujipatia Sh800 milioni

Padri Mbaroni Kwa Ulawiti Paroko mbaroni akidaiwa kughushi, kujipatia Sh800 milioni

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bunda mkoani Mara, Karoli Mganga anatuhumiwa kughushi nyaraka na kujipatia zaidi ya Sh800 milioni kinyume cha sheria.

Paroko huyo anatuhumiwa kuhusika kwenye tukio hilo pamoja na mhasibu wa parokia hiyo, Gerald Mgendagenda.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase alisema kutokana na tuhuma hizo, jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa wote wa wawili na kufanya uchunguzi kwa ajili ya hatua nyingine zaidi.

Alisema tayari jeshi hilo limekamilisha uchunguzi na jalada limepelekwa Ofisi ya Mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi.

Kamanda alisema paroko huyo na mhasibu wake wanadaiwa kugushi nyaraka kwa nyakati tofauti na kujiapatia kiasi hicho cha fedha, mali ya parokia hiyo, kinyume cha sheria na taratibu.

Alisema mbali na kughushi nyaraka, watuhumiwa hao pia wanadaiwa kughushi sahihi za watu mbalimbali, hali iliyowawezesha kufanikisha malengo yao na kujipatia kiasi hicho cha fedha.

“Sisi tumekamilisha upelelezi wetu tangu wiki iliyopita na jalada tumelipeleka kwa mwendesha mashtaka wa Serikali, hivyo tunasubiri hati ya mashtaka kwa ajili ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria," alisema.

Alisema watuhumiwa hao wako nje kwa dhamana wakisubiri kukamilika kwa mchakato wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live