Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa: Maaskofu waliodhalilisha watoto kingono wajisalimishe

32778 Pic+papa Tanzania Web Photo

Fri, 21 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Vatican. Papa Francis ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, amewataka maaskofu katili waliowadhalilisha watoto kingono kujisalimisha.

“Kwa wale walionyanyasa watoto nasema kwamba mjitafakari kisha mjisalimishe mbele za haki za kidinadamu, halafu mjiandae kwa hukumu ya Mungu,” alisema Papa wakati akihutubia baraza la seneti liitwalo Curia kama ilivyo utamaduni wake kuhutubia wakati wa Sherehe za Krismas huko makao makuu Vatican.

Ikiwa bado haijafahamika kwa usahihi kwamba Papa alikuwa akitoa maelekezo hayo kwa ajili ya mfumo wa kimahakama wa kanisa, Serikali au vyote, vyanzo vya habari kutoka Vatican vnaamini hii ni mara ya kwanza  Papa kusema hayo moja kwa moja.

Papa, ambaye awali amekuwa akitumia sherehe za Krismasi kukemea vitendo vya rushwa na uongozi mbaya katika baraza hilo, wakati huu ameangazia zaidi tatizo kubwa la unyanyasaji wa kingono duniani.

“Ifahamike wazi kwamba,wote wanaokabiliwa na machukizo haya, kanisa halitasita kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria, wote waliofanya makosa hayo kanisa halitanyamaza au kutoipa umuhimu kesi yoyote,” alisema.

Alikubali kwamba kanisa lilifanya makosa makubwa kipindi cha nyuma, lakini akaahidi kuwa makosa yaliyofanywa zamani yanatoa nafasi ya kumaliza hilo janga.

Waathirika wa vitendo hivyo vya ngono, wana matumaini ya mkutano huo kuja na sera iliyo wazi ambayo itawafanya maaskofu wenyewe kuwajibika kutokana na kushindwa kushughulikia kesi hizo.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz