Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Panya road wakitu-beep tutawapigia"- Naibu Waziri

Panya Road Panyaaaaa Panya Road

Wed, 11 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi imewataka vijana wanaojihusisha na vikundi vya kihalifu vinavyopora na kujeruhi wananchi katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Dar es Salaam kutafuta kazi nyingine kwani watashughulikiwa ipasavyo.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Mei 10, 2022, Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini, wakati akijibu swali la mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima, lililohusu ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya vikundi vya Panya road vinavyopora na kujeruhi watu.

"Tumeaahidi kushughulika na vijana hawa wakitu-beep sisi tutawapigia, kwahiyo kwa tahadhari hiyo tunaomba watafute kazi nyingine ya kufanya badala ya uhalifu wanaoufanya dhidi ya binadamu hatutawavumilia," amesema Naibu Waziri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live