Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panya road 14 wakamatwa Zanzibar

Panya Road Kortini Panya road 14 wakamatwa Zanzibar

Thu, 13 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana I4 kati yao 6 wakitokea Dar es Salaam wanaodaiwa kujihusisha na uhalifu kwa kutumia silaha za jadi maarufu kwa jina la Panya Road wamefikishwa Mahakamani wakituhumiwa kupora na kujeruhi watu kadhaa Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibu, ACP Richard Thadei Mchomvu amesema kuna makundi mawili ya Panya Road na yote wamefanikiwa kuyadhibiti, mbali na waliofikishwa Mahakamani kuna wengine wanane wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.

"Kila kundi linapojaribu kujitokeza tunalizima kwa kuhakikisha kuwa hawafanyi vile wanavyotaka, kwa leo nilitaka niwaambie kuwa tumefanikiwa kuzima makundi mawili ya hao wanaojiita 'Panya Road' Alisema Kamanda huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live