Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panya Road wavamia Kibaha na kujruhi tisa

PANGA Panya Road wavamia Kibaha na kujruhi tisa

Sun, 20 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi waliovamiwa na kundi la vijana Wahalifu wenye silaha mbalimbali maarufu Panya Road maeneo ya Kibaha Mkoani Pwani wamesema vibaka hao waliwavamia kwa makundi huku wakisema hiyo ndio njia yao ya kupata rizki hivyo kila mtu atii amri ya kutoa anachoelekezwa.

Wakizungumza kwenye makazi yao baadhi ya wahanga na majeruhi wa tukio hilo wameeleza kuwa vijana hao walikuwa wakitamba kuwa hawana ajira na hiyo ndiyo ajira yao, na wao wanachotaka ni fedha, simu na mali nyingine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema wahalifu hao wameiba vitu kadhaa na kujeruhi watu, na mmoja wa majeruhi ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

Daktari wa kitengo cha dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi. Dkt Oscar Feruzi amesema wamepata wagonjwa 9 waliotokana na tukio hilo na wawili wamepelekwa Hospitali ya Muhimbili (Upanga) na Mloganzila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live