Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pamoja na "Presha" ya maandamano, Mbowe kizimbani leo

FREEMAN AIKAEL Mwenyekiti wa CHADEMA,Freema Mbowe

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania,Chama Cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA),Freeman Aikael Mbowe anatarajia kufikishwa mahakamani leo Agosti 6 kusikikiliza mashitaka yanayomkabili.

Mbowe anashitakiwa kwa makosa ya Ugaidi na kupanga njama za kuua Viongozi wa serikali na atafikishwa mahakamni Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka yake.

Wakati huo huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro,amewaonya wanachama wa Chama hicho akisema si ruhusa kufanya maandamano wala kukusanyika katika maeneo ya Mahakama,lakini Viongozi wa CHADEMA wamesisitiza watahudhuria kwa wingi Mahakamani hapo wakati wa kusikilizwa shauri hilo kwa kuwa Mahakama ni muhimili huru na hakuna Sheria inayowazuia watu kusikiliza kesi mahakamani.

Mbowe alikamatwa mwezi uliopita Jijini Mwanza alipokwenda Kuhudhuria Kongamano la Kushinikiza Katiba Mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live