Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Padri asimulia alivyomkuta mshtakiwa akifanya uharibifu kanisani

Picha Mahakama Data Geita Kanisa Padri asimulia alivyomkuta mshtakiwa akifanya uharibifu kanisani

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shahidi wa tano katika kesi namba 62/2023 ya mshtakiwa Elpidius Edward, anayedaiwa kuvamia Kanisa Kuu la Kiaskofu jimbo Katoliki Geita na kufanya uharibifu uliosabisha hasara ya Sh48.2 milioni, ameieleza mahakama namna alivyomkuta mshtakiwa akifanya uharibifu ndani ya kanisa hilo.

Shahidi huyo Padri Charles Kato wa jimbo Katoliki Geita aliieleza mahakama kuwa usiku wa Februari 26, 2023 akiwa amelala alipigiwa simu na mlinzi na kumweleza kuna mtu ndani ya kanisa anayefanya uharibifu wa vifaa.

Akiongozwa na wakili wa Serikali Godfrey Odupoy, Padri Kato aliieleza mahakama kuwa baada ya kupokea simu, alikwenda eneo la tukio na alipofika alikutana na walinzi wengine wanne na kuingia nao ndani ya kanisa na kumkuta mhalifu akifanya uharibifu na kufanikiwa kumdhibiti.

Shahidi huyo alipoulizwa kama mshtakiwa alikuwa na zana zozote alizotumia kufanya uharibifu alidai hakuwa na chochote bali alitumia mikono yake.

Aliileza mahakama kuwa mbali na kufanya uharibifu kwenye eneo la kamera za CCTV, mshatakiwa huyo alikuwa amevunja misalaba, tebernaco, sanamu ya bikira maria pamoja na kung’oa vipaza sauti na kuvitupa na kuondoa vitambaa vya altare pamoja na kiti cha maungamo na kuvunja majaba yanayotunza maji matakatifu.

Alipopewa nafasi ya kuuliza maswali mshtakiwa alitaka kujua sababu za shahidi kutokuja na ushahidi wa kamera ambao ndio utaonyesha uhalisia wa tukio na badala yake amekuja yeye.

Shahidi alidai asingeweza kuja na mfumo huo kwa sababu hajaambiwa, lakini pia akaeleza mshtakiwa aliharibu mfumo mzima wa CCTV Camera.

Mshtakiwa huyo pia alitaka kujua mtu sahihi aliyefungua mlango wa kanisa kutokana na shahidi wa tatu kudai yeye ndiye alikuja na funguo na kufungua kisha walinzi wakaingia kumdhibiti na leo shahidi mwingine akieleza yeye ndiye aliyefungua kanisa hilo.

Kesi hiyo inayosikilizwa na hakimu mwandamizi wa Mahakama ya hakimu mkazi Geita imeahirishwa hadi Septemba 11.

i hiyo inayosikilizwa na hakimu mwandamizi wa Mahakama ya hakimu mkazi Geita imeahirishwa hadi Septemba 11 kwa upande wa mashtaka kuendelea kuleta mashahidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live