Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Operesheni punguza mahabusu yaanza

E6AzDjVXIAMpQ8D.jpeg Operesheni punguza mahabusu yaanza

Sun, 11 Jul 2021 Chanzo: eatv.tv

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo, amesema Serikali imeanzisha Operesheni Maalumu ijulikanayo kwa jina la “Operesheni Punguza Mahabusu” lengo ikiwa ni kupunguza msongamano wa mahabusu katika magereza mbalimbali nchini.

Submitted by Elbogast on Jumapili , 11th Jul , 2021 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo akisalimiana na maaskari wa gereza la Ruanda.

Waziri Khamis Hamza Chilo amesema hayo wakati  akizungumza katika kikao kilichohusisha wafungwa na Mahabusu wanawake  katika Gereza la Ruanda jijini Mbeya.

Mbali na hilo pia aliwapa vitu mbalimbali ikiwemo magodoro, Taulo za Kike, Miswaki na sabuni.  

Chanzo: eatv.tv