Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa wa TRA na askari polisi, kortin kwa kuomba rushwa ya Sh2 milioni

61995 Pic+TRA

Mon, 10 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ofisa Msaidizi wa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charity Ngalawa (28) na askari polisi wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shtaka la  kuomba rushwa ya Sh 2milioni.

Mbali na Ngalawa washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai ni askari polisi  mwenye namba H 4810 PC Ramadhani Uweza( 28) na mwenzake H 4886 PC Simon Sugu( 26), wote kutoka Kituo cha Polisi Osterbay, wilaya ya Kinondoni.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na shtaka moja la  kuomba rushwa ya Sh 2 milioni kutoka kwa mfanyabiashara wa Kariakoo, Ramadhani Ntunzwe.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Sofia Gula amedai leo Jumatatu, Juni 10, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi,  kuwa washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 29, 2016 katika eneo la Kimara Mwisho, Wilaya ya Kinondoni.

Gula amedai  siku hiyo ya tukio, washtakiwa kwa pamoja wakiwa Watumishi wa Umma, walishawishi rushwa ya Sh2 milioni kutoka kwa mfanyabiashara Ramadhani Ntunzwe.

Gula amedai  washtakiwa hao walishawishi rushwa hiyo ili waweze kuachia  mizigo ya mfanyabiashara huyo walioukamata kwa madai kuwa alifanya  udanganyifu wa bidhaa alizonazo na hivyo kuathiri ukadiriaji wa kodi, kazi ambayo ni ya mwajiriwa wake.

Habari zinazohusiana na hii

Washtakiwa baada ya kusomewa shtaka linalowakabili walikana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka umedai kuwa  upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo, wakili wa anayewatetea washtakiwa hao, Ambros Mkwera aliiomba mahakama iwape wateja wake dhamana kutoka na kesi inayowakabili kudhaminika.

Hakimu Shaidi, alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa hao, ambayo ni kila mshtakiwa anatakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye barua inayotambuliwa kisheria pamoja na kitambulisho atakaye saini bondi ya Sh 5milioni.

Washtakiwa wote wamefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huru kwa dhamana.

Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 10,2019, itakapotajwa na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Chanzo: mwananchi.co.tz