Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa wa Polisi na wenzake wadaiwa kuiba Sh600, 000

Hukumu Pc Data Ofisa wa Polisi na wenzake wadaiwa kuiba Sh600, 000

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: Mwananchi

Watu watano akiwemo Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Lidya Ngua wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la wizi wa Sh600, 000.

Akisoma hati ya mashtaka leo Machi 14, Wakili wa Serikali, Caroline Matemu amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na kosa la kumuibia Sofia Liana Mbaga.

Matemu amedai kuwa kati ya Februari 21, 2020 eneo la Charambe Kisutu wilayani Ilala washtakiwa hao walimwomba Sofia Mbaga kiasi cha Sh600, 000.

Amesema upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mkuu Amir Msumi alisema ili washtakiwa hao wadhaminiwe ni lazima kila mmoja awe na mtu mmoja atakayesaini bondi ya Sh 600,000.

Washtakiwa hao walikidhi masharti ya dhamana hiyo na wapo nje kwa dhamana na kesi imeahirishwa hadi Machi 23, 2023 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.

Chanzo: Mwananchi