Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa wa CRDB, wenzake kortini kwa madai ya kumuibia mteja

77569 Crdbpic

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ofisa wa Benki ya CRDB, Andrew Babu na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka nane likiwemo la kuiba na kutakatisha fedha kiasi cha Sh106 milioni.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuiba fedha kwa kutumia kadi ya Viza Gold mali ya Charles Kihamia.

Mbali na Babu, washitakiwa wengine ni William Sige, Justina Boniphas na Ally Tatupa ambao wote wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 101/2019.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amewasomea mashtaka yao jana Alhamisi Septemba 26, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Agustina Mbando.

Simon amedai washtakiwa hao walitenda makosa hayo  kati ya Oktoba 7, 2018 hadi Aprili 29, 2019 katika Benki ya CRDB iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika tarehe hizo, washtakiwa hao waliiba Sh106.26 milioni  mali ya Charles Kihamia.

Pia Soma

Advertisement
Oktoba 29, 2018 katika benki ya CRDB Ubungo, Sige alighushi sahihi ya Kihamia katika fomu ya maombi ya kadi ya Tembo kwa lengo la kuonyesha ni sahihi.

Wakili Simon amedai Sige alighushi sahihi hiyo katika kitabu cha usajili, kadi ya Tembo na katika fomu ya namba ya siri za Kihamia.

Iliendelea kudaiwa kuwa mshtakiwa huyo Oktoba 29, 2018  aliwasilisha kwa ofisa wa benki hiyo, Omary Mduyah fomu ya maombi ya kadi ya Tembo kwa lengo la kuonyesha ni halali ilitolewa na Kihamia.

Katika shtaka la kutakatisha fedha, washtakiwa hao walijipatia Sh106.26 milioni kutoka kwa Kihamia kupitia kadi ya benki ya visa waliyoighushi wakati wakijua fedha hizo ni kosa hilo ni zao la wizi.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi na kesi hiyo bado haujakamilika kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mmbando ameahirisha kesi hiyo hadi  Oktoba 10, 2019 itakapotajwa tena.

Washtakiwa wote walirudishwa rumande kutokana na shtaka la utakatishaji fedha kutokuwa na dhamana.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz