Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa halmashauri kortini tuhuma kuomba rushwa

56937 Pic+takukuru

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Korogwe.Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemfikisha mahakamani mtumishi wa halmashauri ya mji wa Korogwe kwa tuhuma ya kuomba rushwa ya Sh 500,000 na kupokea Sh 200,000 ili asimfikishe kwenye vyombo vya sheria mfanyabiashara aliyekuwa akikopesha fedha bila leseni.

Mtumishi huyo wa halmashauri, Idrisa Shelukindo ambaye ni ofisa mtendaji kata ya Old Korogwe alifikishwa mahakamani juzi.

Ilidaiwa na mwendesha mashtaka wa Takukuru, Barry Galinoma mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Korogwe, Albert Nyang’ali kuwa, Aprili 14 mwaka huu katika kata hiyo mshtakiwa alimtaka Longinus Nchimbi ampe Sh 500,000 ili asimfikishe mahakamani baada ya kumkamata akimtuhumu kufanya biashara ya kukopesha fedha bila leseni.

Mwendesha mashtaka huyo alisema mshtakiwa huyo alifanya hivyo huku akitambua kuwa ni kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Mshtakiwa alikana mashtaka hayo na kesi hiyo iliahirishwa hadiJuni 11 mwaka huu itakapofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali.

Chanzo: mwananchi.co.tz