Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa forodha TRA mahakamani kwa kuomba rushwa ya Sh500,000

74893 Forodha+pic

Mon, 9 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, ofisa forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Peter Mwangamilo kwa kushawishi rushwa ya Sh500,000.

Wakili wa Takukuru, Veronica Chimwanda leo Jumatatu Septemba 9, 2019 amedai mbele ya hakimu mfawidhi, Martha Mpaze kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Septemba 3, 2019.

Amedai siku ya tukio mshtakiwa alimshawishi Leonard Ruvumwa kutoa kiasi hicho cha fedha ili kurahisisha zoezi la uhakiki kwa kampuni ya kutoa na kupokea mizigo ya Maltlines International Tanzania.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikana na upande wa mashtaka kudai upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Mpaze ametoa masharti ya dhamana, kumtaka  mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja sharti ambalo lilitimizwa na mshtakiwa huyo.

Hakimu Mjaya ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 30, 2019 itakapotajwa tena.

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz