Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa elimu afariki dunia kwa kupigwa risasi

Thu, 17 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Ofisa elimu maalum wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Martin Goi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Tukio hilo lililothibitishwa na mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo limetokea juzi jioni Jumatatu Januari 14, 2019 katika mgahawa wa Rhotia Garden mjini Karatu.

Goi alipigwa risasi mbili kifuani na kukimbizwa Hospitali ya Selian mjini Arusha kwa matibabu na kufariki dunia jana Jumanne Januari 15, 2019.

"Nilipewa taarifa na kufika eneo la tukio nilimkuta  mtumishi huyo akivuja damu alikimbizwa kituo cha Afya cha Dabaldi ili kuongezewa damu," amesema Mahongo.

Amewataka wafanyabiashara wilayani humo kufunga kamera za CCTV ili kuwabaini watu wenye malengo ya kufanya vitendo vya kihalifu.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz