Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa LHRC adaiwa kutekwa mchana kweupe Dar

89389 Kutekwa+pic Ofisa LHRC adaiwa kutekwa mchana kweupe Dar

Fri, 20 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ofisa wa kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini Tanzania, Tito Magoti ametekwa na watu wasiojulikana leo mchana Ijumaa Desemba 20, 2019.

Magoti inadaiwa kutekwa akiwa kituo cha mafuta cha Puma kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam na watu sita waliovalia kiraia kisha kumwingiza katika gari na kuondoka naye.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Mussa Taibu amesema hana taarifa za tukio hilo na kuwaomba ndugu za mhusika kutoa taarifa polisi.

Kufuatia tukio hilo, watu mbalimbali wametoa taarifa za kulaani kitendo hicho huku wakiviomba vyombo vya Dola kuingilia kati kumtafuta Magoti.

Katika taarifa yake mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Anna Henga ameeleza masikitiko yake kutokana na tukio hilo na kubainisha kuwa kwa mujibu wa mashuhuda watu waliomchukua Magoti walikuwa na gari aina ya Toyota Harrier rangi ya maziwa na baada ya kumchukua walielekea barabara ya kwenda katikati ya Jiji.

 “Kama LHRC tunakemea vikali vitendo vya utekaji kwani ni mwendelezo wa ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwamo haki ya ulinzi binafsi.”

Chanzo: mwananchi.co.tz