Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa Kilimo kortini kwa kuomba rushwa ya Sh 10,000

Baraza Kageraa Ofisa Kilimo kortini kwa kuomba rushwa ya Sh 10,000

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Njombe imemkamata na kumfikisha Mahakamani Rashid Mkocha ambaye ni afisa kilimo wa kata ya Mlowa halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe kwa tuhuma za kumuomba rushwa ya shilingi elfu kumi (10,000) mkulima ili asajiliwe kwenye kitabu kwa ajili ya mbolea ya ruzuku.

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Kassim Ephrem amesema mtuhumiwa alikamatwa November 9 mwaka huu mara baada ya kupata taarifa kwa raia mwema na kuandaa mtego uliosaidia kumkamata mtuhumiwa.

“Tumemfungulia kesi afisa kilimo wa kata kwa kudai rushwa kwa mwananchi asajiliwe kwenye kitabu ili aweze kupata namba akachukue mbolea ya ruzuku halafu yeye ni afisa kilimo wa kata hata ukimuangalia mkulia unaona dah”amesema Kassim Ephrem.

Ametoa wito kwa kuacha vitendo hivyo kwa kuwa serikali ina nia njema ya kuwasaidia wananchi hivyo hawataweza kusita kumchukulia sheria mtumishi yeyote anayekwenda kinyume na sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live