Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyama ya nyati yampeleka jela miaka 20

68122 Nyara+pic

Wed, 24 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti mkoani Mara nchini Tanzania imemhukumu Marwa Mnanka (45) mkazi wa kijiji cha Nyamakendo kifungo cha miaka 20 kwa makosa ya ujangili.

Akitoa hukumu hiyo leo Jumatano Julai 24, 2019 Hakimu Ismael Ngaile amesema ushahidi wa jamhuri haukuacha shaka na kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka 20 ambayo ni adhabu ya chini kwa mjibu wa sheria  ya wanyamapori namba 5/2009.

Mapema waendesha mashitaka wa Serikiali ya Tanzania, Elisa Benjamini, Emmanuel Zumba na Paskael Nkenyenge katika kesi ya uhujumu uchumi namba 23/2018 wameiambia Mahakama kuwa mshitakiwa alikamatwa Mei 8, 2018 eneo la mto Bologonja ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Wamesema alifikishwa mahakamani kwa makosa matatu ya kuingia ndani ya hifadhi bila kibali, kukutwa na silaha mikuki miwili na kisu kimoja, kosa la tatu ni kukutwa na nyama mbichi ya nyati mwenye thamani ya Sh4,142,000 kinyume cha Sheria.

Wameomba mahakama itoe adhabu kulingana na sheria huku mshitakiwa akiomba asamehewe kwa kuwa ni kosa lake la kwanza.

Chanzo: mwananchi.co.tz