Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyama ya Pundamilia yawapeleka jela miaka 20

52833 Pic+nyama+punda

Wed, 17 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti imewahukumu washitakiwa wawili kila mmoja kifungo cha miaka 20 kwa kukutwa na vipande vinne vya nyama ya Pundamilia.

Waliohukumiwa leo Jumatano Aprili 17,2019 ni Mossi Iranga(45)na Nkiri Chacha(32) wakazi wa kijiji cha Masinki.

Akisoma hukumu Hakimu mkazi Ismael Ngaile amesema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo haukuacha shaka ikiwemo vielelezo walivyokutwa navyo washitakiwa.

Amesema kulingana na mashitaka waliyoshitakiwa nayo  ya uhujumu uchumi kila mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka 20 jela, na kuwa milango ya rufaa iko wazi.

Mapema mwendesha mashitaka wa Jamhuri  Emmanuel Zumba amesema kwa pamoja walikamatwa Machi 11,2018 ndani ya Pori la Akiba la Ikorongo.

Walikutwa na vipande vinne vya pundamilia vyenye thamani ya Sh 2,616,000 kinyume cha sheria na kufikishwa mahakamani kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi la kuingia ndani ya Hifadhi na kukutwa na nyara.

Washitakiwa wameomba mahakama iwaonee huruma kwa kuwa wanategemewa na familia zao.



Chanzo: mwananchi.co.tz