Singida. Aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na wenzake watatu leo Jumatano Mei 29, 2019 wameripoti kituo cha polisi kati mkoani Singida na kutakiwa kwenda tena kituoni hapo Mei 31, 2019 kwa ajili ya mahojiano.
Nusu saa tangu wafike kituoni hapo, walichukuliwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupabana na Rushwa (Takukuru) na kuhojiwa kuanzia saa 3 hadi saa 4 asubuhi, kisha kuachiwa kwa dhamana ya Sh5milioni kila mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Nyalandu amesema baada ya kuhojiwa wametakiwa kuripoti polisi Ijumaa huku Takukuru wakiwataka kuripoti Juni 19, 2019.
Amesema wakiwa polisi hawakuhojiwa zaidi ya kutakiwa kurejea tena Ijumaa
“Inashangaza lakini ninawaomba makamanda wote (wanachama wa Chadema) kuwa na utulivu wasilipe ubaya kwa ubaya ila walipe ubaya kwa wema, “amesema Nyalandu.
Nyalandu alikamatwa na Takukuru Jumatatu Mei 27, 2019 katika kata ya Itaja jimbo la Singida Kaskazini, akituhumiwa kwa makosa mawili ya rushwa na kuendesha mkutano bila kibali.
Habari zinazohusiana na hii
- Takukuru yataja sababu za kumkamata Nyalandu
- Alichokisema Nyalandu baada ya kuachiwa kwa dhamana
- Nyalandu ashangaa kukamatwa kwake, Takukuru wamjibu