Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nuru, Seth na Ezekiel wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Arrested Crime.jfif Nuru, Seth na Ezekiel wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Wed, 16 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma imewatia hatiani washtakiwa Nuru Venevas, Seth Simon na Ezekiel Kalobezi kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji.

Imeelezwa mahakamani hapo mbele ya Jaji Matuma katika kesi ya mauaji Namba 36 ya mwaka 2020 kuwa mshtakiwa Nuru Venevas na wenzake wawili walifanya tukio hilo mnamo tarehe 2 Oktoba, 2016 majira ya usiku katika Kijiji cha Kwaga Wilaya ya Kasulu iliyopo Mkoani Kigoma ambapo walimvamia marehemu na walinzi wenzake wakiwa wanalinda mitambo ya kutengeneza barabara ya Kasulu-Kigoma na kumuua marehemu kwa kumkatakata na panga kisha kuiba control box ya excavator (sanduku la mchimbaji wa barabara) ambayo mshtakiwa Seth Simon alikamatwa nayo Mkoani Geita.

Hukumu hiyo ilitolewa mahakamani hapo baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri pasipo kuacha shaka. na hivyo kupelekea washtakiwa wote watatu kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Kesi hiyo iliendeshwa na Mawakili wa Serikali Robert Magige na Edna Makala, ambapo upande wa utetezi uliongozwa na Sadick Aliki akiwa pamoja na Dennis Kayaga.

MBOWE ALIVYOINGIA MAHAKAMANI, ULINZI MKALI, HUKUMU YA MDUDE CHADEMA

Chanzo: millardayo.com